Chorus
Huyu Baba gani, una kichaa!!!
Chagua kati ya wale anayekufaa!
Baba hana haki, amezubaa,
Baba hana haki!!!!!, unakataa? x3
Versi 1
Nani kama mama, maneno ya mtaani,
Baba kwa mama, haoni ndani,
Afanye wafanyavyo, hajulikani,
Kawa mkiwa, hana nuru usoni,
Kila jambo lake, mzigo mzito kichwani,
Kila kwenye mafanikio, anatajwa mama,
Kila kwenye uozo, ni baba siyo mama,
Kuitwa baba majukumu, pia kubeba lawama,
Kufa kupona juu yako, sifa ziende kwa mama,
Chorus
Huyu Baba gani, una kichaa!!!
Chagua kati ya wale anayekufaa!
Baba hana haki!!!!!, unakataa? x3
Versi 2
(Women voice) Mbona sipati mimba?
Lawama kwa baba,
Ukweni kuna shida,jukumu la baba,
Shuleni kuna changamoto, mwambie baba,
Kazi imeyumba, hakuna dogo, unachanganya baba,
Mke apendeze, ale vizuri, komaa baba,
Watoto wakue na siha njema, fahari ya baba,
Mafanikio ya kwa ujumla, nani kama mama,
Usife moyo, kaza buti, Dunia itasimama,
Watoto silaha, za kumuangamiza baba,
Ustawi wa jamii, unamkaba haki baba,
Keki anaitiwa mama, kulea haki finyu kwa baba,
Dunia Hadaa ulimwengu shujaa, baba juu ya msalaba,
Dunia ina nia gani,
Baba ana fundi gani,
Kilio chake kama samaki, machozi yaishia majini,
Haki finyu kwa baba, samaki mtungoni,
Wao wanawezeshwa, kumkaba baba kooni,
Baba ni mnyonge, mnyongeni
Abadani , asilani haki yake mpeni
Baba hana haki!!!!!, unakataa? x3