Oooow ni sharikan tenaaah
Usiku silali, namuomba Mungu anilindiye wazazi wangu
Kidogo nachopata kwa jasho langu, niitunze familia yangu
Nahizi shida aah, tumeumbiwa wanadamu
Lakini natabasamu, nikiamka kila asubuhi salama
*(Pre-Chorus)*
Niliahidi moyo wangu, siwezi kulala njaa
Nitapambana hadi mwisho, hata nikikosa njia
Na machozi yangu ni dua, kwako Baba wa milele
Niweze kuwapa ndoto, hata bila kulelewa
---
*(Chorus – Hook)*
*Ee Mungu, nitie nguvu, nisisimame njiani*
*Nijaalie baraka, nifike mbaliii
*Mapambano ni mengi, lakini moyo bado upo*
*Na ndoto zangu zinaishi, hata nisipokuwa nazo*
ila bado ,bado naamini nitatoboa
---
*(Verse 2)*
Sikuwahi pata urahisi, lakini sikuwahi kata tamaa
Nilijifunza kuamka, hata wakati machozi yamejaa
Sauti ya mama ikiniambia, “Mwanangu usilegee,”
Ndio maneno ninayobeba, kila nikiteleza nayaelewa
*(Bridge)*
Siku moja nitainuka, watu waseme "alijitahidi"
Watoto wangu watakula matunda ya maumivu yangu
Siishi kwa makuu, naishi kwa neema
Na kila jasho linalodondoka ni hatua ya baraka
Ni sharikan tenaaaah wa ngare hiii