[Verse 1]
Tangulia Mwokozi kaonekane
Katika njia zangu niziendeazo
Onyesha mapito kwa watesi wangu
Kaonekane uko mbele yangu
[Chorus]
Ukiwa na mimi sina shaka
Ukiniongoza ni salama ahaa
Uwepo wako Bwana ni kinga tosha
Na nguvu zako ni ushindi kaonekane
[Verse 2]
Tunapita nyakati mbaya zenye
Kutisha pia hutukatisha tamaa
Ila twajua kua wewe uko mbele
Umetuahidi kwamba hutaniacha
[Chorus ]
Ukiwa na mimi sina shaka
Ukiniongoza ni salama ahaa
Uwepo wako Bwana ni kinga tosha
Na nguvu zako ni ushindi kaonekane