nakuite rafiki ushiriki, ni yangu furaha furifuri,
imekuwa yangu ashiki, sifa zake kama uturi,
sauti nyingi za uluwa, na hoja kwake za arudhi,
heri ningemwona, nimpe langu pambaja.
sauti za shubiri kwake, nakemea tena mkome,
lake jina ndivyo alivyo, kweli ni suluhu,
heri ningemwona, nimpe langu pambaja,
nimzawadie johari na lulu, toka moyoni mwangu.
siha njema, dua safi namwombea,
Jalia mruzuku maono mufti, hekima pia,
kazi vema kafanya, basara ni dira kwake kazini,
tunu zetu tena zitunzeni, adhimu umati utakuzidishieni.
sauti za shubiri kwake, nakemea tena mkome..
lake jina ndivyo alivyo, kweli ni suluhu,
heri ningemwona, nimpe langu pambaja,
nimzawadie johari na lulu, toka moyoni mwangu.