[Verse]
Kama uua la kondeni likosapo jua zuri
Najitosa ukumbini, mambo yako kifikiiri
Najikuta bondeni, na ukiwa forifori
Wanikana muhibaka, sababu mi kitale?
Ewe penzi nipulika, ingawa unateule
[Chorus]
Mm nakuwaza ooh nawazia inavyohisi kuwa nawe.
Uu nakuwaza, ooh naimajin, mawazo yako juu yangu.
[Verse]
Umenichokora chokora unyago
Umenivingirisha kama gogo
Umenifanyisha kazi isiyo yangu baby
Umenifanya mwavuli kikinyesha
Umenifanya bonzo wa kuchekesha
Maombi yangu siachi kuyatuma
[Chorus]
Mm nakuwaza ooh nawazia inavyohisi kuwa nawe.
Uu nakuwaza, ooh naimajin, mawazo yakoo juu yangu.
Njaribu kukuongelesha dada
Nimejaribu, Kukuona ni shida
Sijui Umbo lako li kwa mnada?
Napitapita angaa. Nionekane
Nakuitaita dakika kwa nyingiine
Na sijui umekuwa bubu au kipofu...
Je wataka niogelee kuvuka bahari Hindi
Ama niukwee kilimanjaro
[Chorus]
Mm nakuwaza ooh nawazia inavyohisi kuwa nawe.
Uu nakuwaza, ooh naimajin, mawazo yakoo juu yangu.
Kwako wewe ntaridhika, huba lako la milele
Soni kwangu imeshika, nione lako umbile
Takuwa kwangu talaka, ntakapopata batile
Ewe kipenzi nipulika, ingawa una teule