Mwanadamu kazaliwa, kutoka tumbo la mama,
Siku zake duniani, zinahesabika daima.
Maisha ni mafupi, yamejaa taabu,
Kila kukicha mapambano, yasiyoisha burudani.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Kama ua linavyochanua, na papo hapo kukauka,
Ndivyo uhai wetu, unavyopita kama moshi.
Kama kivuli kipitacho, kisicho na msimamo,
Maisha yetu haya, yanayoyoma kwa haraka.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Huibuka kama ua, la kupendeza macho,
Lakini hukatwa ghafla, bila huruma wala machozi.
Hukimbia kama kivuli, hakina pa kukaa,
Hivyo ndivyo maisha, yanavyopita haraka sana.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Mungu umeinuka, kutufumbulia macho,
Kutupa ufahamu, wa maisha mafupi haya.
Basi unatuletea, hukumuni mbele zako,
Tukiwa dhaifu hivi, tusio na nguvu zetu.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Ijapokuwa udhaifu, umetutawala sisi,
Na hatuna nguvu zetu, za kujitetea wenyewe.
Bado tunasimama, mbele ya kiti chako,
Kutoa hesabu yetu, ya yote tuliyotenda.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Lakini Bwana Mungu, wewe umejaa rehema,
Neema yako yatutosha, kutuvusha katika dhiki.
Hata tukiwa dhaifu, wewe unatupa nguvu,
Kuyatimiza mapenzi, yako maishani mwetu.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele
Hivyo basi twasema, maisha ni safari fupi,
Lakini tuna tumaini, katika wewe Mwokozi.
Tutavuka milima, tutavuka mabonde yote,
Tukijua kuna uzima, milele na milele.
Siku zetu chache, maisha kama ua,
Lakini tuna tumaini, kwa Mwokozi wetu Bwana.
Hata tukipita, katika bonde la uvuli,
Atatupokea kwake, uzima tele milele